HATUA ZA KUHAKIKISHA MATUNDA NA MBOGAMBOGA NI SALAMA NA AFYA KUTOKA SOKONI HADI MEZANI.
Matunda na mboga ni chakula bora kwa afya. Hata hivyo, je, unajua kuwa vijidudu hatari kama Salmonella, E. coli, na Listeria vinaweza kuwepo kwenye matunda na mboga? Kuna hatua muhimu zinazoweza kukusaidia kubaki salama na kuhakikisha matunda na mboga unazotumia ni salama kuanzia sokoni hadi mezani.
Usalama wa Matunda na Mboga Unapokuwa Dukani au Sokoni.
✅. Angalia Michubuko na Madoa.Chagua matunda na mboga ambazo hazijachubuka au kuwa na madoa yaliyoharibika, isipokuwa kama unapanga kuzipika.
✅. Hakikisha Matunda na Mboga Zilizokatwa Zinahifadhiwa Kwenye Baridi.
Chagua matunda na mboga zilizokatwa na kufungashwa ambazo zinahifadhiwa kwenye jokofu au kwenye barafu.
✅. Tenganisha.
Tengisha matunda na mboga mbali na nyama mbichi, kuku, na samaki kwenye toroli la dukani na kwenye mifuko ya manunuzi au ya kuhifadhia.
Usalama wa Matunda na Mboga Unapoyatayarisha Nyumbani.
✍️ Nawa Mikono.
Nawa mikono kabla na baada ya kuandaa matunda na mboga.
✍️. Osha Matunda na Mboga.Osha au sugua matunda na mboga chini ya maji yanayotiririka kabla ya kula, kukata, au kupika.
Matunda na mboga yenye lebo ya “pre-washed” hayahitaji kuoshwa tena nyumbani.
✍️Tengisha Vifaa na Maeneo ya Kupikia.
Hifadhi matunda na mboga mbali na (si karibu au chini ya) nyama mbichi, kuku, na samaki kwani vinaweza kumwaga juisi zenye vijidudu.
✍️Tumia ubao maalumu (cutting board) kwa matunda na mboga ambao hautatumikakukatia nyama, kuku au samaki.
✍️Osha ubaoni, meza, na vifaa kwa maji ya moto yenye sabuni kabla na baada ya kuandaa matunda na mboga.
✍️. Hifadhi Kwenye Baridi.
Hifadhi matunda na mboga zilizokatwa, kuchumwa au kupikwa kwenye jokofu.
Zingatia unachokula maana ndo afya yako
By Neema




