Jumamosi, 16 Aprili 2022

Mradi wa Utambuzi kuhusu umuhimu wa AFYA ya Akili mpaka ukomo wa sasa

MRADI WA UTAMBUZI KUHUSU UMUHIMU WA AFYA YA AKILI NA TIBA SAIKOLOJIA KATIKA JAMII YA SASA MPAKA UKOMO WA JAMII YA SASA

Maana ya Afya ya Akili

Afya ya akili inahusu ustawi wa mtu katika ngazi tatu ambazo ni:

  1. Nafsi na Utashi
  2. Akili na fikra
  3. Mwili na Hisia

Hivyo mtu anavyo hisi/ waza na kusimamia wazo ndivyo anavyo tenda katika maisha yake.

SIFA ZA MTU MWENYE AKILI TIMAMU

  1. Kujitambua katika maisha
  2. Kufikiri tofauti na mazoea
  3. Kukumbuka na kuelewa
  4. Kushirikiana na watu wengine
  5. Kujifunza na kujisimamia
  6. Kuhimili changamoto za maisha
  7. Kutatua matatizo
  8. Kutumia vipawa na kalama vyema

VYANZO VYA MAGONJWA YA AKILI KWA MTU

  1. Ugumu wa maisha
  2. Madawa ya kulevya
  3. Michezo ya kamali
  4. Ajari
  5. Magonjwa ya mda mrefu
  6. Mazingira
  7. Mila na desturi za kijamii

DALILI ZA MAGONJWA YA AKILI

  1. Mfadhaiko
  2. Kupoteza kumbukumbu
  3. Kujitenga kwa muda mrefu
  4. Kuwa na hasira za haraka wiki mbili +
  5. Kujidhalau na kukatatamaa
  6. Kushindwa kutimiza majukumu

NAMNA YA KUKABILIANA NA MAGONJWA YA AKILI

  1. Kulielewa tatizo au chanzo, hili ni la kwanza
  2. Kudhibiti msongo wa mawazo
  3. Kuepuka vyanzi hasi kuhusu watu
  4. Kufanya mazoezi ya mwili na akili
  5. Kupata lishe bora katika maisha
  6. Kuepuka matumizi ya dawa za kulevya
  7. Kutumia tiba saikolojia
  8. Kutunza afya ya mazingira kupata hewa safi

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

15 Comments:

  1. Hakika kazi ya ukombozi wa fikra ni jukumu letu sote

    JibuFuta
  2. ZIPI NI Aina za magonjwa ya Afya ya akiki?

    JibuFuta
    Majibu
    1. Kuna ya kuzaliwa nayo
      Kuna ya kupata kimakuzi

      Mfano.

      sonona
      Ni ugonjwa wa Akili ambapo mtu husikikia huzuni mara kwa mara na huambatana na mawazo hasi.

      Wasiwasi
      Hii hutokea kw mtu kulingana na matendo na mazingira alipo na huwanihali ya kupindukia.

      Na mengine kama bipolar
      Skizofrenia
      Usonji

      Futa
  3. Yeah, ni jambo la kheri kutumia taaluma na tunu zetu kwa ajili ya ukombozi wa jamii yetu.

    JibuFuta
  4. Kazi nzuri San πŸ€πŸ™

    JibuFuta