MEZA YA FUNZO ITAMBUE AFYA YA AKILI KATIKA FAMILIA.
Dalili za ugojwa wa sonona ni pamoja na;
🔷️Kuwa na huzuni sana, kukosa matumaini na kukata tama ya kuishi
🔷️Kuhisi upweke, kujilaumu, kujitenga na wengine na kuwa na fikra hasi
🔷️Kuwa na hasira za karibu na kukasirishwa hata na mambo madogo
🔷️Kupoteza hamu ya kufanya mambo ambayo mtu alikuwa akiyafurahia kabla kama muziki, michezo au kutizama filamu
🔷️Kukosa usingizi au kulala kupita kiasi
🔷️Kukosa nguvu na kuchoka haraka
🔷️Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito kwa wengine kuongezeka hamu ya kula na kuongezeka uzito
🔷️Kupata shida kufikiri, kukumbuka vitu na kufanya maamuzi
🔷️Kutamani kufa, kufikiria kujiua na kujaribu kujiua.
🔷️Kuwa na maumivu ya viungo kama kuumwa kichwa au mgongo
Sonona ikiwa kali zaidi, mgonjwa huanza kusikia sauti za watu wakimsema vibaya na kumkatisha tamaa. Sauti hizi huwa kichwani kwake na watu wengine hawawezi kusikia.
Endapo wewe mwenyewe au mtu wako wa karibu ataonyesha dalili za sonona ni vyema akapatiwa msaada, maana sonona isipodhibitiwa inaweza kupelekea mtu kujidhuru au kujitoa uhai.
Tutumie meseji inbox kwa msaada zaidi na shida yako kupitia,
akiliplatform9@gmail.com
WhatsApp no 0626 551 859 Akili Platform Tanzania
Tazama Tafakari Tenda kwa busara tunza afya ya akili na Mazingira ulipo •usijidhuru wala kudhuru maisha yako au ya mwingine.






Umenena ukweli kabisaaaaa
JibuFutaSomo nzuri
JibuFuta