Jumatano, 30 Aprili 2025

Nawezaje kujitambua kuwa nina tatizo la akili?

Habari za majukumu Hongera kwa shughuli za ujenzi wa taifa katika kufikia maendeleo endelevu ya secta mbalimbali hasa ulipo.

Mpiga picha baada ya kupigwa picha na mpiga picha katika mjadala wa kujadili namna ya kutokomeza janga la watu kujitoa uhai
Team Akili Platform Tanzania mkoa wa Dar es salaam ikiongozwa na Ndg Bahati Laizer _ Mratibu wa Mkoa.

Maswali ya msingi katika kujiuliza kila wakati.

Je wiki mbili zilizo pita mpaka sasa unapitia hali ya kupoteza msukumo wa ndani wa kufanya vitu ulivyokuwa unavipenda?

Je umekuwa ukihisi huzuni na kupata hali ya kutaka kukata tamaa kwa hizi wiki mbili zilizo pita mpaka sasa?

Je unasumbuliwa na hali ya kutokupata usingizi ukilala au unajikuta unalala kuliko kawaida kwa hizi mbili zilizo pita?

Je umejikuta ukiwa na uchovu sana muda mwingine kuishiwa nguvu kabisa?

Je unapatwa na hali ya kujiona huna thamani au unaona kama hauna jipya katika maisha yako ya sasa?

Je unapatwa na hali ya kuzungumza peke yako wakati unatembea njiani? 


Akili Platform Tanzania tunakukumbusha kama majibu yako ni ndiyo maswali 4 kuendelea unashauriwa kutafuta msaada wa kitaalamu kutoka kwa wasaikolojia .

Kama hujui unawapataje tuwasiliane 0626 551 859 WhatsApp au 0764 246 072 kawaida.

Tazama Tafakari Tenda kwa busara tunza afya ya akili na Mazingira ulipo.

Afya ya akili ni nguzo muhimu katika kufanikisha ndoto za kila mmoja wetu tuijali Sana.

Imetolewa na Utawala Akili Platform Tanzania makao makuu mkoa wa Tabora wilaya Tabora mjini kata ya kitete mtaa wa Community nyumba no 5.

Follow 

          Akili Platform Tanzania

 mitandaoni upate mambo mazuri.

0 Comments:

Chapisha Maoni