Jumamosi, 10 Mei 2025

10.05.2025

 

TAARIFA YA MREJESHO YA USHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 63 YA TANZANIA RED CROSS SOCIETY

Tarehe: 10 Mei 2025

Mahali: Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma

Mgeni Rasmi: Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania( Mhe Dotto Biteko amewakilisha)

Kauli Mbiu: Kudumisha Ubinadamu

Akili Platform Tanzania imepata fursa ya kushiriki katika maadhimisho ya miaka 63 ya Tanzania Red Cross Society yaliyofanyika tarehe 10 Mei 2025, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma. Hafla hii muhimu iliudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na wadau wa ubinadamu, ikiwa ni pamoja na Mgeni Rasmi, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lengo la Ushiriki:

Ushiriki wa Akili Platform Tanzania ulikuwa na malengo yafuatayo

_Kuimarisha ushirikiano na mashirika mengine yanayojishughulisha na masuala ya kibinadamu

_Kuonesha mchango wa Akili Platform Tanzania katika sekta ya afya ya akili, uhifadhi wa mazingira, na haki za binadamu

_Kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu mbinu bora za kuhudumia jamii.

Uongozi wa Ushiriki:

Akili Platform Tanzania iliongozwa na Mratibu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Bertila Mtitu, pamoja na timu yake. Waliwakilisha shirika kwa weledi na kuonesha dhamira ya kweli ya kudumisha ubinadamu.

Shughuli Zilizofanyika:

  1. Kushiriki kwenye mijadala na maonyesho ya kazi za kibinadamu.
  2. Kushiriki katika maombi ya pamoja na hotuba za viongozi mbalimbali kuhusu kudumisha ubinadamu.

Mafanikio:

  1. Kujenga mtandao wa ushirikiano na mashirika mengine, ikiwa ni pamoja na Tanzania Red Cross Society.
  2. Kutambulisha juhudi za Akili Platform Tanzania katika ngazi ya kitaifa.
  3. Kuongeza uelewa wa washiriki kuhusu umuhimu wa kujitolea.

Changamoto:

  1. Wakati wa muda mfupi wa maonyesho kulinganisha na idadi kubwa ya washiriki.
  2. Mahitaji makubwa ya taarifa kutoka kwa washiriki wa maonesho.

Mapendekezo:

  1. Kuandaa mipango ya awali kwa ajili ya matukio kama haya ili kuongeza ufanisi wa ushiriki.
  2. Kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha masuala ya kibinadamu yanapewa kipaumbele.

Hitimisho:

Akili Platform Tanzania inatoa shukrani za dhati kwa Tanzania Red Cross Society kwa kutoa nafasi ya kushiriki katika maadhimisho haya muhimu. Tunajivunia kuwa sehemu ya juhudi za kudumisha ubinadamu na tunatarajia kushiriki tena katika shughuli zijazo zinazolenga kuimarisha ustawi wa jamii yetu.

Imetolewa na:

 Akili Platform Tanzania











0 Comments:

Chapisha Maoni