Alikuwepo mvulana yatima aliyekuwa akiuza vitu vidogo kutoka nyumba hadi nyumba ili kuishi na kulipia masomo yake.
Siku moja alikuwa na njaa kali sana na hakuwa na nguvu kabisa, kwani alikuwa hajala chochote kwa siku tatu na hakufanikiwa kuuza chochote.
Kisha akaamua: "Katika nyumba ile ya jirani, ni lazima niombe chakula, na njaa inanitesa sana."
Alipofika, akagonga mlango: ngo ngo ngo!
Akatokea msichana mrembo, na akamwambia kwa upole:
"Karibu, kuna nini?"
Mvulana alipomuona yule msichana mrembo wa rika lake, akapata aibu ya kuomba chakula. Akasema kwa hofu:
"Habari dada!"
"Msichana akajibu, nzuri kaka!"
Mvulana akaanza
"Ee...eeh......naweza kuomba maji kidogo tafadhali?"
Yule msichana akasema kwa upole akimtazama machoni:
"Kaa hapa, nakuja."
Aliingia ndani, akarudi na keki mbili kubwa na kikombe cha maziwa, pamoja na kikombe cha maji juu ya sinia.
Akamwambia:
"Hatukuwa bado tumetayarisha chakula, lakini tafadhali pokea hivi kwa sasa, vitulize njaa yako... na hapa ni maji uliyoyaomba."
Mvulana alishindwa kusema chochote ila kwa sauti ya unyenyekevu:
"Asante sana dada yangu!"
Baada ya kula na kunywa, akauliza:
"Dada, jina lako nani?"
"Jina langu ni Mariam... Mariam Josiane."
"Uligunduaje kuwa nina njaa?"
Akamjibu:
"Sababu mbili. Kwanza, bibi yangu alikuwa anasema, 'Macho ni kioo cha moyo' – macho husema mengi kuliko mdomo. Pili, wazazi wangu walinifundisha:
'Mpatie mkate na maziwa anayekuomba chai.'
Ndiyo sababu."
"Na wewe, jina lako nani?"
"Mimi ni Ahmed."
"Sasa unaweza kusubiri chakula chetu."
Kijana akasema,
"Hapana dada, hiki kimenitosha kabisa, naomba niondoke."
Msichana aksema, sawa hakuna neno.
nimefurahi kukujua... Mungu akufanikishe."
na kijana akasema,
"Asante kwa moyo wako wa dhahabu, tenda wema daima, Mungu atakulipa."
Miaka ikapita...
Wazazi wa Mariam walifariki, akabaki na mdogo wake peke yao.
Siku moja Mariam akaumwa, na madaktari wakagundua ana saratani ya mfuko wa uzazi (uterine cancer).
Daktari akamshauri afanye upasuaji haraka kwenye hospitali kubwa.
Akasema:
"Nina euro laki tatu tu, zitatosha?"
"Hatujui, lakini jaribu bahati yako."
Wakaenda jijini kutafuta matibabu. Kwa sababu ya dharura, akafanyiwa upasuaji mara moja – bili ilikuja baadaye: Euro milioni 2.5!
Hakuwa na mtu wa kumsaidia, wala mali ya kuuza.
Akalazwa hospitali kwa wiki mbili zaidi kwa kushindwa kulipa.
Siku moja asubuhi, muuguzi akaja na bahasha – ndani yake kulikuwa na karatasi ya kuruhusiwa kutoka hospitalini na barua.
Akaanza kulia alipoiona. Akafungua barua:
"Habari dada!"
"Nzuri kaka!"
"Ee...eeh...naomba maji tafadhali..."
"Kaa, nakuja... hatujapika bado, lakini chukua hiki kwa sasa... na hapa ni maji yako."
"Asante, tenda wema siku zote, Mungu atakulipa."
Alikumbuka kila kitu. Akalia kwa sauti.
Mdogo wake akamuuliza:
"Mariam, unalia nini? Kuna nini?"
Akamjibu kwa sauti ya huruma:
"Tendea kila mtu wema, hata usiyemjua – siku moja Mungu atakulipa."
Mwisho wa barua iliandikwa:
"Tarehe 1 mwezi ujao, unaweza kuanza kazi hapa hospitalini, kama utakubali.
Bili yako imelipwa kikamilifu kwa kikombe cha maziwa...
–By Dkt. Ahmed ."
Akalia tena kwa furaha, akakubali kazi. Na akapona kabisa.
Ujumbe:
Tenda wema bila kutarajia malipo. Wema haupotei.
Panda asubuhi, mchana na jioni – hujui ni mbegu ipi itachipuka.
Ni hadithi ya kugusa moyo yenye mafunzo makubwa ya utu, ukarimu, na kulipwa kwa wema.

0 Comments:
Chapisha Maoni