Ijumaa, 23 Mei 2025

REPORT YA USHIRIKI WA AKILI PLATFORM TANZANIA KATIKA WIKI YA NYUKI KITAIFA 2025

 RIPOTI YA USHIRIKI WA AKILI PLATFORM TANZANIA KATIKA WIKI YA NYUKI KITAIFA - DODOMA (17-20 MEI 2025)

Utangulizi
Shirika la Akili Platform Tanzania limeshiriki Wiki ya Nyuki Kitaifa iliyofanyika mkoani Dodoma tarehe 17 hadi 20 Mei 2025. Maonyesho haya yaliwaleta pamoja wadau mbalimbali wa sekta ya ufugaji nyuki na wahifadhi mazingira ili kujadili fursa na changamoto zinazohusu sekta hiyo.

Malengo ya Ushiriki

  1. Kukuza uelewa kuhusu huduma zinazotolewa na Akili Platform Tanzania.
  2. Kujifunza na kubadilishana maarifa kuhusu sekta ya ufugaji nyuki.
  3. Kushirikiana na wadau wa sekta hii kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Shughuli Zilizofanyika Maonyesho ya Huduma za Shirika Akili Platform Tanzania ilionesha huduma zake zinazohusiana na afya ya akili, uhifadhi wa mazingira, na haki za binadamu. Banda letu lilivutia washiriki wengi, wakiwemo wadau wa sekta ya nyuki, wanafunzi, na viongozi wa serikali.





Kutembelea Mabanda ya Maonyesho Wajumbe wetu walitembelea mabanda mbalimbali ili kujifunza mbinu bora za ufugaji wa nyuki na kuongeza maarifa juu ya matumizi ya bidhaa za nyuki.


Ushiriki katika Mjadala wa Nyuki na Fursa Zake Shirika lilishiriki katika mjadala maalum uliolenga kuelewa mchango wa nyuki katika mazingira na uchumi. Fursa mpya na changamoto katika sekta hii zilijadiliwa.


Ziara ya Mafunzo kwa Vitendo
a) Tulitembelea eneo la Swahili Honey ambapo tulijifunza mbinu za kisasa za uchakataji wa asali.

b) Tulishiriki ziara maalum kwa Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu, na kumpa zawadi kama shukrani kwa mchango wake katika maendeleo ya sekta ya nyuki.





Kuwakaribisha Viongozi na Washiriki Mbalimbali Banda letu lilitembelewa na viongozi mashuhuri, ikiwa ni pamoja na viongozi wa serikali na washiriki wengine wa maonyesho. Hii ilisaidia kujenga mahusiano mapya kwa maendeleo ya pamoja.









Matokeo na Mafanikio

  • Shirika limeongeza maarifa juu ya sekta ya nyuki na tumefungua fursa.
  • Tulipewa cheti cha ushiriki na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kutambua mchango wetu kama wadau wa afya ya akili na mabadiliko ya tabia nchi katika juhudi za kuongeza thamani katika zao la nyuki na kupambana na magonjwa yasiyo ambukizwa.
  • Tumepata fursa ya kushirikiana na wadau wapya.
  • Shirika limepokea maoni chanya kutoka kwa viongozi waliotembelea banda letu.
  • Tulifanikiwa kusikiliza na kuchambua hotuba ya Mgeni Rasmi ambaye alikuwa Mhe Kassim Majaliwa _ Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwanzo hadi mwisho.




Hitimisho
Ushiriki wa Akili Platform Tanzania katika Wiki ya Nyuki Kitaifa mkoani Dodoma ulikuwa wenye mafanikio makubwa. Tunatarajia kushiriki zaidi katika maonyesho kama haya ili kuendelea kuimarisha juhudi zetu za kuhifadhi mazingira na kukuza uchumi wa kijani.

Nb. Mapendekezo

  1. Kuendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya nyuki kwa maendeleo endelevu.
  2. Kuandaa programu za mafunzo kwa wanachama na jamii kuhusu ufugaji bora wa nyuki.
  3. Kuhakikisha ushiriki endelevu katika matukio ya kitaifa yanayohusiana na malengo ya shirika.

0 Comments:

Chapisha Maoni