Jumamosi, 24 Mei 2025

VIJANA ZAIDI 30 WAPIGWA MSASA JUU YA DHANA YA AFYA YA AKILI 24.05.2025 MKOANI TABORA_ MWEZI WA UELEWA JUU YA AFYA YA AKILI.

Ripoti ya Semina ya Vijana: Kanisa la Moroviani, Parishi ya Ipuli


Tarehe: Jumamosi, 24 Mei 2025
Mahali: Parishi ya Ipuli, Manispaa ya Tabora

Mada Kuu: Afya ya Akili kwa Kijana

Washiriki wa Akili Platform Tanzania_ waliofika katika Kanisa hilo kuwakilisha Shirika.

  • Balozi Yoshua Kiteta: Mtoa Mada
  • Madam Asti Nyagawa: Mchangia Mada
  • Ndugu Edgar Milanzi: Mchukua Matukio (Camera Man)

Muhtasari wa Semina

Vijana zaidi ya 30 walihudhuria semina hii muhimu iliyolenga kuwapa elimu juu ya afya ya akili. Mada zilizojadiliwa ni pamoja na:

  1. Afya ya Akili ni nini?
  2. Kutambua dalili za changamoto ya afya ya akili.
  3. Mbinu na mikakati ya kuboresha, kutunza, na kulinda afya ya akili.
  4. Namna sahihi ya kumsaidia mtu mwenye matatizo ya afya ya akili.
  5. Athari za Dawa za Kulevya na utupaji hovyo taka.

Madam Asti Nyagawa alihimiza vijana kujihusisha na kazi za mikono, kama vile ujasiriamali, ili kujenga uhuru wa kifedha na kupunguza utegemezi. Pia, aliwakaribisha vijana wa kanisa hilo kutembelea ofisi za Akili Platform Tanzania kwa mafunzo ya kama 

Kazi ni kipimo cha utu
  • Utengenezaji wa sabuni za maji
  • Mafuta
  • Keki
  • Biskuti
  • Batiki

Madam Asti aliahidi kutoa mafunzo hayo kwa wahusika kuandaa vitendea kazi kwa lengo la kuwasaidia vijana kuwa wachangiaji wakubwa katika maendeleo ya taifa.

Shukrani kutoka kwa Kanisa

Mchungaji wa kanisa, Mchungaji Emmanuel Chelehani, aliipongeza Akili Platform Tanzania kwa mchango wao mkubwa katika elimu ya afya ya akili. Alisisitiza umuhimu wa afya ya akili katika maisha ya kiroho na kijamii, huku akiahidi kushirikiana na shirika hilo kwa siku zijazo.

Shukrani za Akili Platform Tanzania kwa mchango wa wanao thamini uwepo wetu kama wadau wa afya ya akili, mazingira na haki za binadamu. 

Tunawashukuru kwa dhati taasisi zote za serikali, binafsi, na za kidini zinazotuunga mkono. Ushirikiano huu unatuimarisha na kutupa nguvu ya kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa jamii.

Mawasiliano


0 Comments:

Chapisha Maoni