Jumanne, 29 Julai 2025

Mafunzo ya kutatua changamoto ili kujali afya ya akili.

 WANANCHI MKOA WA TABORA WATAKIWA KUTONYANYAPAA WENYE CHANGAMOTO ZA AFYA YA AKILI

Wananchi wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kuacha vitendo vya unyanyapaa dhidi ya watu wanaokumbwa na changamoto za afya ya akili, na badala yake kutambua kuwa kundi hilo linahitaji msaada, upendo na kuthaminiwa kama sehemu ya jamii.
Rai hiyo imetolewa na Roghat Robert, Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali Akili Platform Tanzania, wakati wa mafunzo ya siku moja yaliyowakutanisha walimu, vijana, wazazi na wanafamilia wote waliokuwa tayari kujifunza na kubadilika kimaisha iliyokutanisha vijana 30 katika Ukumbi mdogo wa Ofisini kuu ya Akili Platform Tanzania mkoa wa Tabora Halmashauri ya Tabora mjini kata ya kitete mtaa wa Community nyumba no 5

Sauti Roghat 1:
“Tunaitaka jamii kutenga muda katika familia zao kwa ajili ya kufanya huduma ya unasihi ndani ya familia, ili kusaidia kuimarisha afya ya akili ya watoto, vijana na watu wazima.”

Aidha, Roghat ametoa wito kwa serikali na wadau wa afya kuhakikisha kila mkoa unakuwa na wataalamu wa saikolojia kwa kushirikiana na Maafisa Ustawi wa Jamii, ili kutoa huduma za kisaikolojia kwa wananchi wanaokumbwa na changamoto mbalimbali za kimaisha.

Sauti Roghat 2
“Vijana wetu wanahitaji huduma sahihi za msaada wa kisaikolojia. Tunapendekeza serikali ihakikishe kila mkoa unakuwa na wataalamu wa saikolojia, wanaoweza kuwasaidia kwa karibu.”
Ndg. Roghat F. Robert, Mkurugenzi wa Akili Platform Tanzania, alisisitiza umuhimu wa kuwekeza kwenye lishe asilia na kutenga muda kwa ajili ya afya ya akili. Aliahidi kuandaa mafunzo mengine ya kufungua mwezi wa nane.

Maoni ya Vijana:
“Ni mara ya kwanza kuhisi kuwa na utulivu kwa njia ya asili” 
“Tunaomba mafunzo haya yafike mashuleni na vyuoni” 

_Taarifa imeandaliwa na:_ 
Akili Platform Tanzania
Kwa mawasiliano: 0626 551 859 au 0764 246 072 kwa maendeleo jumuishi. 

0 Comments:

Chapisha Maoni