Ripoti ya Uchaguzi wa Mfanyakazi Bora wa Mwaka 2024/2025
Utangulizi Katika jitihada za kuhakikisha kwamba Akili Platform Tanzania inapata mfanyakazi mwenye ujuzi na sifa zinazolingana na malengo ya shirika, tumezingatia vigezo muhimu wakati wa mchakato wa uteuzi wa mfanyakazi bora wa mwaka 2024/2025.
Vigezo Vilivyotumika Mchakato wa uteuzi wa mfanyakazi bora ulizingatia vigezo vifuatavyo:
- Uadilifu na Maadili ya Kazi: Kuonyesha uwajibikaji, uaminifu, na ufuatiliaji wa maadili ya shirika.
- Uelewa wa Maeneo ya Shirika: Maarifa na shauku ya kuchangia maendeleo ya afya ya akili, mazingira, na haki za binadamu.
- Uwezo wa Mawasiliano na Ushirikiano: Kufanya kazi vizuri ndani ya timu na kushirikiana na wadau.
- Ujuzi wa Utatuzi wa Matatizo na Ubunifu: Kufanikisha majukumu kwa ubunifu na suluhisho bora.
- Elimu na Uzoefu: Mafanikio katika taaluma au mafunzo yanayohusiana na kazi za shirika.
Matokeo ya Uteuzi Baada ya mchakato wa tathmini, tunapenda kutangaza kuwa Ndg. Asti Jackson Nyagawa ameibuka kuwa mfanyakazi bora wa mwaka 2024/2025.
Majukumu na Mafanikio Ndg. Asti Jackson Nyagawa aliteuliwa kwa nafasi ya Usimamizi wa Idara ya Kazi za Mikono, ambapo alifanya kazi kubwa ya:
- Kusimamia idara ya kazi za mikono kwa weledi mkubwa.
- Kuwahamasisha na kuwafundisha vijana zaidi ya 50 kupata ujuzi wa kazi za mikono.
- Kutoa elimu ya afya ya akili kwa vijana, ambayo ilichangia kuboresha ustawi wao wa kiakili na kijamii.
Hitimisho Tunatoa pongezi kubwa kwa Ndg. Asti Jackson Nyagawa kwa mafanikio haya makubwa. Tunatarajia kwamba juhudi zake zitaendelea kuleta matokeo chanya kwa shirika letu na jamii kwa ujumla.
Na hii itakuwa chachu ya kufikia mafanikio endelevu ya secta mbalimbali katika jamii.
Imetolewa na:
Usimamizi wa Akili Platform Tanzania
2025-05-01





0 Comments:
Chapisha Maoni