Ijumaa, 2 Mei 2025

TAARIFA NJEMA

@TPSC _TABORA _ KITOVU CHA UZALISHAJI WATUMISHI MAKINI zaidi ya 1500 wapatiwa elimu ya afya ya akili. 

Mwezi Mei ni mwezi wa Uelewa juu ya Afya ya Akili, na Shirika la Akili Platform Tanzania linapongeza Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) kwa kutambua na kuthamini umuhimu wa somo la afya ya akili kwa wanafunzi wake.

“Afya ya akili siyo ugonjwa,” amesema Mkurugenzi wa Shirika la Akili Platform Tanzania, Bw. Roghat F. Robert, leo tarehe 2 Mei alipokuwa akizungumza na vijana wa Chuo cha TPSC.

Ameeleza kuwa hata unapokumbana na changamoto za kisaikolojia, ni muhimu kutambua kwamba hauko peke yako.

“Usione aibu kutafuta msaada wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu,” amesisitiza.

Katika mafunzo yake, Bw. Robert amefundisha dhana ya afya ya akili, akionyesha mambo yanayoweza kuathiri afya ya akili na hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kudhibiti changamoto hizo.

Aidha, ametoa wito kwa vijana kutojihusisha katika matumizi ya vileo, sigara, na dawa za kulevya ambazo zina madhara makubwa kwa afya ya akili.

“Kujali afya ya akili ni kujali maisha yako; chagua maisha yenye afya kwa kuachana na tabia zinazoharibu afya yako,” amesema Bw. Robert kwa msisitizo.

Tazama, tafakari na tenda kwa busara. Tunza afya ya akili na mazingira ulipo.


0 Comments:

Chapisha Maoni