Jumatatu, 19 Mei 2025

Wiki ya Nyuki kitaifa 2025

USHIRIKI WA MAONYESHO YA WIKI YA NYUKI KITAIFA


Akili Platform Tanzania inapenda kuwataarifu wananchi wote kuwa tayari tupo katika Maonyesho ya Wiki ya Nyuki Kitaifa yanayoendelea mkoani Dodoma, katika viwanja vya Chinangali, kuanzia tarehe 17 Mei 2025 hadi 20 Mei 2025.


Chief akiwa banda letu 

Katika maonyesho haya, tunawakaribisha wageni wote kutembelea banda letu ili kujifunza zaidi kuhusu:

Afya ya Akili Tutaelimisha jamii juu ya umuhimu wa afya ya akili na jinsi ya kudhibiti msongo wa mawazo katika maisha ya kila siku.

Huduma zetu za ushauri na elimu ya afya ya akili zitapatikana.

Mabadiliko ya Tabianchi Tutaeleza jinsi mabadiliko ya tabianchi yanavyoathiri maisha ya binadamu na mazingira, hususan sekta ya kilimo na ufugaji wa nyuki.

Tutatoa elimu ya mbinu endelevu za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Matunda ya Asili, Hususan Gogondi Tutaonyesha faida za matunda ya asili, ikiwa ni pamoja na Gogondi, na jinsi yanavyosaidia kuboresha afya ya mwili na akili. Pia, tutashirikisha bidhaa za asili zinazotokana na nyuki kama asali na nta.

Huduma Maalum:

  • Meza  ya kielimu kuhusu afya ya akili.
  • Kuonja na kununua bidhaa za asali safi na ya asili kutoka kwa nyuki wadogo na wakubwa.

Tafadhali jisikie huru kutembelea banda letu na kushiriki nasi katika kuleta mabadiliko chanya kwa jamii zetu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia namba ya simu 0626 551 859 au barua pepe akiliplatform9@gmail.com.

Karibuni wote tushirikiane kuleta afya bora ya akili, mazingira endelevu, na kutumia zawadi za asili kwa ustawi wa maisha yetu!

Imetolewa na: Akili Platform Tanzania


0 Comments:

Chapisha Maoni