Tunaamini kila mtu ni kiongozi ila siyo kiongozi anajua Uongozi wake ⏰
Kazi kubwa sana ya Akili Platform Tanzania ni kuwa kusaidia kufia jamii sehemu ambayo inakuwa haijafikiwa na serikali sasa ukitazama Vizuri utaona kuwa serikali inaweka mazingira ya ramani na sisi wadau tunaongezea yetu.
Soma vipaumbele vyote utaona cha Afya ya Akili, na tiba asili hakuna tiba asili bila utunzaji wa mazingira.
Akili Platform Tanzania tunafanya kazi kote nchini Tanzania, tukilenga zaidi mikoa ya Tabora na maeneo yenye uhitaji mkubwa. Tunaendesha shughuli zetu kupitia semina, mafunzo, na kampeni za uhamasishaji.
Shirika letu linashughulika na makundi mbalimbali ya watu, yakiwemo vijana, wanawake, watoto wenye ulemavu, na jamii kwa ujumla.
Tunawasaidia vijana kuelewa umuhimu wa afya ya akili na kuwapa mafunzo ya ujasiriamali ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea. Kwa wanawake, tunatoa msaada wa kisaikolojia, mafunzo ya haki za binadamu, na mbinu za kutunza mazingira.
Pia tunajihusisha na huduma za lishe na msaada wa kisaikolojia kwa watoto wenye ulemavu na familia zao. Kwa jamii kwa ujumla, tunatoa elimu ya uhifadhi wa mazingira na hatua za kuchukua ili
kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Kazi yetu inalenga kuunganisha jamii katika eneo la kufikia maendeleo endelevu ya afya ya akili na uhifadhi wa mazingira kwa sababu tunatambua kuwa ustawi wa binadamu unahusiana moja kwa moja na mazingira tunayoishi.
Kila mmoja anawajibu na haki ya kujua afya ya akili yake kwa kutambua uwezo wake, udhaifu wake, kipaji chake, Mihemuko yake na mambo yanayohusisha hisia na mihemuko kwa ujumla kupitia matendo.
Kumbuka
Kutunza mazingira ni wajibu wetu na jukumu letu pamoja ila je unajua kuwa mazingira bora ni fursa?
Karibu sana wapendwa kujiunga na Shirika la Akili Platform Tanzania hasa vijana, watumishi na wanajamii.
0764 246 072 au 0626 551 859 roghatfalme@gmail.com au akiliplatform9@gmail.com
Link ya kujisajili kuwa Mwanachama.
https://docs.google.com/forms/d/1l4K0oTtMYx9dDAmczwUkAvgneqm3eAr0GO245srh0Vw/viewform




0 Comments:
Chapisha Maoni