Shirika la AKILI PLATFORM TANZANIA LASHIRIKI MKUTANO WA WADAU WA MALEZI, MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO.
(i) Tarehe: 11/06/2025
(ii) Eneo: UKUMBI MDOGO WA OFISI YA MKUU WA MKOA WA TABORA
Ujumuishi katika malezi inahusisha maeneo yafuatayo;
i. Lishe bora- miaka (0-8) lishe inatakiwa kuzingatiwa ili kukuza miili na Akili zao. Pia mtoto anatakiwa kunyonya miaka (0-2) na sio kukatisha maana inasaidia katika maendeleo ya mtoto.
ii. Malezi yenye mwitikio- Mama mjamzito na mume kutambua ujauzito ili waweze kumpatia mtoto huduma toka akiwa tumboni hadi kuzaliwa kwake. Pia mzazi kuwa karibu na mtoto haswa katika kipindi cha likizo ili kumpatia stadi za maisha.
iii. Ulinzi na usalama wa watoto- mtoto anatakiwa kulindwa katika kipindi chote cha maisha yake zidi ya majanga mbalimbali mfano; ukatili na unyanyasaji wa kijinsia. Hapa ndugu Anord aliongeza kuwa elimu kuhusu ukatili na unyanyasaji itolewe kwa jamii nzima bila kubagua jinsia, maana kila mtu ana wajibu wa kumlinda mwenzake.
iv. Fursa za ujifunzaji wa awali- mtoto ujifunza kutoka kwenye familia, wazazi, mitandao ya kijamii, runinga, jirani na watoto wenzake. Mzazi unatakiwa kuangalia mwanao anajifunza nini kutoka kwa majirani na marafiki zake, kama kizuri kiendelezwe na kama kibaya kikatazwe.
v. Afya bora- mtoto anatakiwa apate chakula chenye virutubisho(MLO KAMILI) vyote kila siku ambayo itamsaidia kukua kimwili na kiakili.
Waandaaji wa tukio: JIDA & OFISI YA AFISA USTAWI WA JAMII MKOA WA TABORA.
Washiriki: MAAFISA MAENDELEO, AFISA LISHE MKOA, WADAU WA MALEZI, MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI, WAZAZI NA WALEZI WA WATOTO WETU.
Mada kuu: SERA NA SHERIA KWA MAENDELEO NA USTAWI.
Mapendekezo (wawasilishaji na wasikilizaji)
i. Bodaboda waache kupakia watoto wengi kwenye pikipiki moja ili kulinda usalama wa watoto wetu mfano kujikinga na ajali. Pia bodaboda wakiona wamebeba wanafunzi watembee mwendo wa taratibu taratibu.
ii. Watoto kipindi cha likizo waachwe wapumzike ili waweze kujifunza kazi za mikono na dini sio kuwapeleka tution.
iii. Wazazi waanze kujitambua kuwafundisha watoto mambo ya dini ili waweze kuwa na maadili mema ya kiulimwengu. Lakini pia ukiona maadili ya mtoto sio mazuri usihukumu kwa haraka bila kujua wanaolea hao watoto wapo aje. kwahiyo wazazi wanahitaji sana elimu ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali kwa mtoto.
iv. Kuzingatia mila na desturi za kitanzania kwenye malezi ya watoto wetu sambamba misingi ya dini iende sambamba. Yaani watoto wawe na hofu ya mungu.
v. Kuwahusisha watoto kwenye michezo mbalimbali maana michezo na fursa kwa uchumi wa mtoto. mfano, kujenga vituo vya michezo kwa watoto ili kuwajengea uwezo mapema.
vi. Kufuata sera mbalimbali zinazomlinda mtoto ili kuweza kufanikisha malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto.
vii. Wizara kuwa na chuo cha kitaifa cha kutrain wataalamu wa day care ili kupata walezi na walimu kwaajili ya maisha ya baadaye. walimu wengi sio walezi maana wanawapeleka watoto kishule shule wanasahau kinyumbani nyumbani.
viii. Kusajili vituo vya Day care ili viweze kutambulika kisheria, endapo likitokea la kutokea litatuliwe. Maana serikali inatambua mchango wao katika ustawi wa jamii kwasababu wanatekeleza mambo ambayo serikali haiwezi kutekeleza yote.
ix. Kusoma sera na miongozo inayoelezea watoto ili kustawisha makuzi, malezi na maendeleo ya awali kwa watoto.
x. Watoa misaada wajikite pia kuwawezesha hao wazazi kimaarifa na kiujuzi ili waweze kujitegemea wenyewe kwa muda mrefu na sio kusubiri tu misaada iwafike.
Mafunzo
i. Mtoto anatakiwa kupatiwa huduma jumuishi za malezi(lishe toshelevu, afya bora, ulinzi na usalama, ujifunzaji wa awali na malezi yenye mwitikio) ili kufikia ukuaji wake timilifu.
ii. Watoto wenye ulemavu wanahitaji huduma za malezi na makuzi kulingana na mahitaji yao. Mfano viziwi wafundishwe kwa kutumia alama.
iii. Kuzifikia jamii zilizopo vijijini ili kuweza kuzifikia. Tusiishie kuwapa misaada tu bali tuwaandae kwaajili ya kujitegemea wao.
iv. Watoto wapewe likizo kama ilivyopangwa na serikali ili waweze kupumzisha akili zao. Pia mtoto akitoka shuleni jioni usimuunganishe aende tena (TUTION CENTRE) bali mfundishe hata kutengeneza bustani au stadi zingine za maisha ili vimsaidie mtoto huko mbeleni.
Hitimisho
Malezi ni jukumu la wote; Mwanaume shiriki kikamilifu kujenga kesho bora ya mtoto wako.
Wote kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya "MTOTO WA AFRIKA" yatakayofanyika wilaya ya skonge tarehe 16/06/2025.
TAFAKURI: Mlee mwanao kama ulivyolelewa wewe mzazi ili aje kuwa kama wewe maana huko mbele atakuwa na maisha yake.
Shukrani
Shukrani kwa mwenyezi Mungu kwa kutupatia neema ya uzima. Pongezi nyingi ziende kwa MKURUGENZI WA AKILI PLATFORM TANZANIA MWL/MC ROGHAT FALME ROBERT kwa kuniamini kijana wake makini kabisa kumuwakilisha kwenye hii event, maana imekuwa ni fursa ya kukutana na watu wapya ili kujifunza na kuongeza uelewa kuhusu Ujumuishi katika malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.
Pia imenisaidia kufungua fursa za kijamii, kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi.
Imeandaliwa na;
ANORD ODO HYERA
BALOZI KUTOKA OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI Akili Platform Tanzania akiliplatform9@gmail.com



Hongera sana sana
JibuFuta