Alhamisi, 7 Agosti 2025

USIPOTEZE TUMAINI LAKO 2025

 Siku ya Mwisho, maisha yetu yatapimwa si kwa mali tuliyojilimbikizia au heshima tuliyopewa, bali kwa athari ambayo tumekuwa nayo kwa maisha ya wengine.  Mungu hatatuuliza kuhusu majina yetu makubwa au vyeo vyetu vya hadhi, bali jinsi tulivyotumia fursa, vipaji, na rasilimali alizotupa kwa manufaa ya wengine.

Maisha sio kile unachoweza kupokea, lakini kile unachoweza kutoa.  Ulitumiaje hekima yako kuwasaidia wale waliopoteza mwelekeo?  Umetumiaje talanta yako kuwainua wengine?  Ulitumiaje muda wako kuwafariji walio na huzuni?

Hakuna aliyeumbwa bila kusudi.  Kila mmoja wetu amepewa uwezo wa kipekee wa kuwa nuru kwa wengine.  Vipaji vyako, mali yako, hata maneno yako - yote ni mbegu ambazo unaweza kupanda kwa kizazi chako na cha wengine.

 Maisha ya kweli na yenye maana ni yale yanayogusa, kuboresha, na kubariki maisha ya wengine.  Hekima ya maisha ni kuishi kwa kutoa.  Kila nafasi ya kusaidia ni nafasi ya kuonyesha upendo wa Mungu kupitia matendo yako.

 

Mwisho wa safari sio juu ya kile ulichopokea, lakini_USIPOTEZE TUMAINI LAKO.

Kuna wakati ambao kitu pekee ambacho utabakia nacho maishani mwako ni TUMAINI (Hope).

Yaani, kila utakachoangalia kwenye maisha yako kitakuwa hakiendi kama ulivyotarajia. Utazungukwa na hali kupoteza, kufeli na kuumia. Kiufupi, hakuna dalili inayoonesha kuwa utafanikiwa.

Ukijaribu kuangalia kuhusu watu unaowafahamu, wengi hautawaona unapowahitaji. Ni kama itakuwa wamekususa vile. 

Hakuna atakayekuuliza unaendeleaje na hata wale ambao watakuwa wanajua hali yako ni kama hawajishughulishi kabisa kukusaidia hata kama wana uwezo.

Watu wengi sana wamekata tamaa katika kipindi cha namna hii. Wengi wamepoteza ndoto zao na kubakia watu wa kawaida. Usiwe mmoja wao.


Hapo ulipo poteza vyote ila usipoteze Tumaini lako. Hicho ndio kitu pekee ulichobakia nacho.

Makao makuu mkoa wa Tabora Halmashauri ya Tabora mjini kata ya kitete mtaa wa Community nyumba no 6.
0764 246 072 
0626 551 859 
roghatfalme@gmail.com 


0 Comments:

Chapisha Maoni