Jumatano, 7 Mei 2025

KAMPENI DHIDI YA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA NA AFYA YA AKILI VYUONI – AKILI PLATFORM TANZANIA YAZINDUA HATUA MPYA

 KAMPENI DHIDI YA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA NA AFYA YA AKILI VYUONI – AKILI PLATFORM TANZANIA YAZINDUA HATUA MPYA

Katika jitihada za kuimarisha afya ya akili na ustawi wa vijana nchini, Akili Platform Tanzania ilipata nafasi ya kutembelea ofisi za Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Kanda ya Ziwa. Ziara hii ilitoa fursa ya kipekee kukutana na viongozi wa kanda na kujadili masuala muhimu kuhusu njia bora za kuelimisha vijana dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.

Mojawapo ya mambo makubwa yaliyosisitizwa ni athari za dawa za kulevya kwenye mfumo wa fahamu wa binadamu. Matumizi ya dawa hizi si tu yanaharibu afya ya akili na kimwili, bali pia yanadhoofisha uwezo wa vijana kufikia malengo yao ya kitaaluma na kijamii.

Kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Akili Platform Tanzania imejizatiti kufanikisha kampeni mbalimbali vyuoni, zenye lengo la:

  1. Kutoa elimu sahihi kuhusu athari za dawa za kulevya.
  2. Kujenga uelewa wa kisheria kuhusu madhara ya kujihusisha na matumizi au usambazaji wa dawa za kulevya.
  3. Kuchochea mijadala ya kijamii kuhusu njia bora za kukabiliana na changamoto hii.
  4. Kuwezesha vijana kushiriki kikamilifu katika kutoa taarifa na kusaidia juhudi za mamlaka zinazohusika.

Tunawaalika vijana wote, viongozi wa vyuo, na wadau mbalimbali kushirikiana nasi katika kuhakikisha elimu sahihi inawafikia walengwa. Kupitia juhudi za pamoja, tunaweza kujenga jamii yenye afya bora, isiyo na matumizi ya dawa za kulevya.

Kwa taarifa zaidi kuhusu kampeni zetu, tafadhali tembelea blog yetu:
akiliplatformtz.blogspot.com

Elimu sahihi kwa ustawi wa kizazi kijacho!
#SayNoToDrugs #AkiliPlatformTanzania


picha ya pamoja 

2 Comments:

  1. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  2. Dawa za kulevya zina athari kubwa kwa mtu binafsi, familia, na jamii kwa ujumla. Athari hizi zinaweza kuwa za kiuchumi, kiafya, kijamii, na kiusalama....

    Jinsi ya kukabiliana na Janga la DAWA za Kulevya
    ✔ Elimu na uhamasishaji shuleni, makanisa, misikitini, mitandaoni
    ✔ Vyombo vya usalama kuweka nguvu kwenye kudhibiti usafirishaji na uuzaji
    ✔ Kuanzisha vituo vya tiba na ushauri (rehabilitation centers)
    ✔ Kushirikisha familia, shule, viongozi wa dini na serikali

    Utumiaji wa Dawa za kulevya ni janga linaloathiri kila sekta ya jamii – kiafya, kiuchumi, kijamii, na kimaadili. Kukomesha tatizo hili kunahitaji ushirikiano wa jamii nzima, kuanzia familia, serikali, taasisi za elimu na viongozi wa kijamii.

    Hayo ndio MAONI yangu na Asante Kwa Makala hii Muhimu katika jamii Yetu Kwa kuileta ili tuweze kushiriki kutoa MAONI

    JibuFuta